Na Mwandishi wetu Dodoma
Kampuni ya Alliance Life Assurance Ltd imeandika historia mpya katika sekta ya bima nchini baada ya kuzindua rasmi ofisi yake ya mauzo jijini Dodoma, hatua inayoiweka kama kampuni ya kwanza ya bima ya maisha kuwa na uwepo rasmi katika Makao Makuu ya nchi.
Uzinduzi huo umefanyika katika hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya bima, akiwemo Meneja wa Mipango na Utafiti wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Edgar Shao, aliyemwakilisha Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo A. Saqware.
Akizungumza katika hafla hiyo, Shao aliipongeza Alliance Life Assurance kwa hatua hiyo, akibainisha kuwa ni ishara ya wazi ya dhamira ya kampuni hiyo katika kusogeza huduma za bima ya maisha karibu zaidi na wananchi, hususan katika kuongeza upatikanaji na uelewa wa huduma hizo nchini.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Alliance Life Assurance Ltd, Byford Mutimusakwa, amesema kufunguliwa kwa ofisi hiyo mpya ni sehemu ya mkakati mpana wa kampuni ya kupanua huduma zake nchini, pamoja na kuleta suluhisho bunifu za bima ya maisha zinazolenga kuwasaidia Watanzania kujenga usalama wa kifedha kwa sasa na baadaye.
Mutimusakwa alibainisha kuwa uwepo wa ofisi hiyo Dodoma utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani, sambamba na kuboresha utoaji wa huduma za ushauri wa kifedha na bima.
Ofisi hiyo mpya iko katika Ghorofa ya Kwanza ya Jengo la Kisangani, Barabara ya Majengo, jijini Dodoma, na inatarajiwa kuwa kitovu muhimu cha huduma za bima ya maisha kwa wananchi wa eneo hilo na maeneo ya jirani.
Aidha, kampuni hiyo imewahimiza wananchi kujitokeza katika ofisi hiyo mpya kupata elimu na ushauri wa kitaalamu kuhusu huduma mbalimbali za bima ya maisha zinazolenga kulinda mustakabali wa kifedha wa familia na jamii kwa ujumla.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...