Katika juhudi za kutoa ajira na kuinua uchumi wa vijijini, Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imefanikiwa kuuwezesha mradi wa Uuzaji wa Maziwa ya Ng’ombe katika Kijiji cha Msasa, Kata ya Runzewe Magharibi.

Mradi huu unaendeshwa na Kikundi cha MAZIWA BORA-MSASA kilichoanzishwa mwaka 2021 na wanachama 5: Wanaume 2 na Wanawake 3. Baada ya kuona bidii yao, Oktoba 2025 Halmashauri ilikifanyia usajili rasmi

Katika mwaka wa fedha 2025/2026, Halmashauri ilitumia asilimia 10 ya mapato ya ndani kutoa mkopo wa Tsh. 15,000,000/= kwa kikundi hiki kwa kipindi cha miaka miwili.

Hii ni sehemu ya mkakati wa serikali kuhakikisha fedha za wananchi zinawagusa moja kwa moja.

Ili mradi uwe na nguvu zaidi, *Shirika la Heifer International liliunga mkono kwa kutoa ruzuku ya Tsh. 27,807,500

Hivyo kufanya thamani kamili ya mradi kuwa ni Tsh. 42,807,500.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe bi Adelina Mfikwa amesema kuwa halmashauri inaendelea kukipatia kikundi hicho mafunzo mbalimbali ili kiweze kuongeza uzalishaji na bidhaa nnyingi zinatokana na maziwa.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Mbogwe kwa namna inavyowajalu wananchi wake hususani katika mikopo ya vikundi.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...