ZAIDI ya Bilioni saba (7) zimekamilisha ujenzi wa soko la kimataifa la mazao katika kijiji cha Kanondo halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Akizungumza wakati akikagua eneo la soko la kimataifa la mazao Waziri wa katiba na sheria Juma Homera ameitaka halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuanza kutumia soko hilo ifikapo August mosi mwaka huu.
Amewapongeza halmashauri kwa kusimamia na kukamilisha mradi huo huku akiwasisitiza kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kwa uwazi na uadilifu.
Aidha mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Frenk Lupimo ameeleza umuhimu wa soko hilo kuwa linauwezo wa kuchukua tani 19,000 na litasaidia kukuza mapato ya ndani na kukuza uchumi kwa wafanyabiashara watakao tumia soko hilo.
Kwa upande wao wananchi wa eneo hilo wamemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa soko la mazao na kuwa soko hilo linakwenda kutatua changamoto na kuondoa walanguzi waliokuwa wakiwaibia wakulima.
Pia wameeleza kuwa awali walikuwa wakiibiwa na walanguzi kutoka nchi jirani wakitumia vipimo vinavyo waumiza wakulima ambapo kwa kujengwa kwa soko hilo tatizo hilo linakwenda kumalizika kwasababu wakulima na wafanyabiasha watauza na kununua mazao katika soko hilo.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...