Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi anayesimamia huduma za Utalii na Masoko, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Mariam Chuma Kobelo, ametunukiwa tuzo ya Iconic Woman in Tourism Promotion katika hafla ya Ladies Talk Awards & Dinner 2026 iliyofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Morogoro.

Bi Mariam ametwaa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza na kutangaza utalii wa Tanzania kupitia ubunifu wa kampeni za masoko, usimamizi wa huduma za utalii, pamoja na juhudi za kukuza utalii wa ndani na wa kimataifa kupitia eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Kupitia uongozi wake, Ngorongoro imeendelea kujijengea sifa kama moja ya vivutio vya utalii wa kifahari (Premium destination) vinavyoongoza barani Afrika, na kusimamia utekelezaji wa kampeni mbalimbali za masoko zinazolenga kuongeza idadi ya watalii na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika maendeleo ya utalii endelevu.

Utambuzi huo unaongeza rekodi ya mafanikio ya kamishna Kobelo, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutafuta masoko mapya ya utalii wa Ngorongoro ndani na nje ya nchi, pamoja na kuratibu programu zinazochangia ukuaji wa sekta ya utalii na kuimarisha juhudi za uhifadhi.

Kamishna Mariam Kobelo ameishukuru Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro chini ya usimamizi wa kamishna wa uhifadhi wa mamlaka hiyo Abdul-Razaq Badru kutokana na ushirikiano mkubwa katika kukuza vipaji vya watumishi na kuviendeleza.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...