Mkuu wa Wilaya ya Mufindi mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa akiwa ameongozana na viongozi wa Mufindi ametembelea na kukagua maonesho ya 88 Mkoa wa Iringa katika Eneo la Kihesa Kilolo Iringa.
Amesema wajasiriamali wengi wana bidhaa bora ambazo zinatakiwa kutangazwa kwa nguvu ili bidhaa hizo zipate masoko nje ya Nchi na Mikoa mbalimbali .
Aidha amekagua teknolojia mbalimbali ambazo zipo kwaajili ya kurahisisha ubareshaji wa utendaji wa kazi wa mkulima au mfugaji katika maonesho hilo na kushauri ziuzwe kwa gharama nafuu ili wakulima na wafugaji waweze kumudu na kuboresha shughuli zao.
Aidha katika maonesho hayo Dc-Mufindi amepata fursa ya kutembelea banda la Halmashauri ya Mji Mafinga na kuweza kuzungumza na wakulima na wafugaji akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella na Mwenyekiti wa Mji Mafinga, Mheshimiwa Regnant Kivinge.



.jpeg)




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...