Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Shirika la  Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO, CPA Jeremiah Mugeta, amesema Kilimo kinamchango mkubwa katika uchumi wa nchi, kwa mujibu wa Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba kilimo pekee kinachangia zaidi ya asilimia 26 katika pato la Taifa, jambo ambalo ni kubwa na lakujivunia na kuona namna ambavyo ushirika unachangia kwenye maendeleo ya uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Julai 8, 2026, Mugeta amesema mchango wa sekta ya ushirika katika maendeleo ya uchumi ni mkubwa, ambapo mazao yanayouzwa kupitia vyama vya ushirika huchangia zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 kwa mwaka, jambo linaloonesha umuhimu wa ushirika katika kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumzia suala la ukaguzi wa vyama vya ushirika amesema wamejipanga kuhakikisha ushirika unazidi kuwa imara, na wauhakika huku malengo Yao na mipango Yao ni kuhakikisha wanaushirika wanapata elimu bora pamoja na misingi na kanuni na taratibu za kuendesha vyama vya ushirika, 

Aidha CASCO kila mwaka huwa wanaandaa taarifa ya jumla ya kuonyesha matokeo ya jinsi ambavyo vyama vya ushirika vilivyofanya shughuli zake kila mwaka, na kutoa maoni katika ukaguzi wanaoufanya.

Vilevile amebainisha mpango walionao katika mwaka wa fedha 2026/2027, wamejipanga kuhakikisha vyama vyote vya ushirika vinakaguliwa ili kuweza kuwapa fursa wanaushirika kujua maendeleo ya shughuli wanazofanya kwenye vyama hivyo, 

Ameeleza mkakati uliopo ni kushirikiana na Tume ya maendeleo ya ushirika, kuhakikisha vyama na viongozi wa vyama vya ushirika wanapata taarifa Sahihi ya watu gani watakaguliwa na ukaguzi huo unatarajiwa kuanza mwezi huu wa Julai kuanzia tarehe 20.

Ametoa wito kwa wanaushirika ni kuhakikisha wanaandaa taarifa za fedha za mwaka 2025/2026 na kuziwasilisha katika ofisi za COASCO zilizopo kwenye mikoa Yao ili ukaguzi uwafikie kwa wakati,  na wahakikishe wanazingatia sheria na kanuni za kuandaa taarifa za fedha ili kupunguza hati chafu katika ukaguzi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...