Jane Mwakyoma-Rukwa.
SERIKALI imetoa siku kumi na nne (14) kwa halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa kuanza kutoa huduma za matibabu kwa wananchi katika kituo cha Afya Chala .
Akitoa maagizo hayo Waziri wa katiba na sheria Juma Homera baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Chala amesema baadhi ya mjengo yamekamilika hakuna budi kuanza kufanya kazi na wananchi waendelee kupata huduma katika kituo hicho.
Amesema serikali ya awamu ya sita imejizatiti kuhakikisha huduma za Afya zinatolewa karibu ili kuondoa kero na adha ya kufuata huduma hiyo mbali na makazi ya wananchi.
Aidha Homera ameonya watumishi wa Afya wanaojichukulia fedha kwa wananchi kinyume na taratibu kuacha kuwatoza fedha na badala yake wafanye kazi kwa weledi na kinidhamu na kufuata taratibu zilizowekwa.
Akiwasilisha gharama za ujenzi kwa Waziri wa katiba na sheria Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Emmanuel Masaga amesema walipokea fedha sh. 250,000,000 kwaajili ya ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD), choo cha nje na kichomea taka .
Aidha amesema mradi huo unatekelezwa kwa kutumia mfumo wa FORCE ACCOUNT ambapo mradi huo upo hatua ya umaliziaji na fedha iliyotumika ni shilingi 248,391,255.13 ikiwa fedha iliyobaki shilingi 1,608,744.87 kwaajili ya malipo ya fundi ujenzi.
Pia Masaga amemshukuru Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 290,669,216.98 katika kituo hicho.
Kwaupande wake diwani wa kata ya Chala Bosco Wazamani amemshukuru Dk. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazofanya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora na za uhakika.
Amesema kujengwa kwa kituo cha Afya katika kata hiyo ni ukombozi tosha kwa wananchi na itakwenda kutatua changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
.jpeg)


.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...