Mkuu wa Wilaya ya Moshi Godfrey Mnzava amefanya ziara katika Kijiji cha Umbwe Kati, Kata ya Kibosho Magharibi, Tarafa ya Kibosho, na kutatua mgogoro wa muda mrefu uliohusiana na ubainishaji wa barabara.
Mgogoro huo ulitokana na baadhi ya wananchi kutokubaliana na ubainishaji wa barabara uliofanywa na Kamati ya Maendeleo ya Kata. Kutokana na hilo palitokea kutokuelewana kuhusu mipaka halisi ya barabara hiyo.
Katika ziara hiyo Mnzava alisikiliza pande zote zinazohusika. Kwa kushirikiana na wananchi na viongozi wa eneo hilo alisimamia zoezi la ubainishaji wa mipaka ya barabara. Uamuzi huo ulikubaliwa na wananchi wenye maeneo yanayopitiwa na barabara, ambao walikubali kuachia eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya umma.
Barabara hiyo inatumika na wananchi kufika Kituo cha Afya cha Umbwe. Inasaidia pia katika shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii katika eneo hilo.
Akizungumza na wananchi baada ya zoezi hilo, Mnzava amewataka kuendelea kudumisha umoja, amani na mshikamano. Amesema maendeleo ya jamii yanategemea wananchi kuweka mbele maslahi ya pamoja.
Wananchi wa Umbwe Kati wamesema wameridhika na jinsi mgogoro huo umetatuliwa na wameahidi kushirikiana na viongozi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...