Na Janeth Raphael - MichuziTv
Tanzania na Misri zimefikia makubaliano ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za kilimo na mifugo, hatua inayotarajiwa kufungua ukurasa mpya wa uwekezaji kupitia maendeleo ya Ranchi ya Ruvu na matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji wa chakula.
Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam, Julai 18, 2026, baada ya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisema nchi hizo mbili zimekubaliana kuongeza ushirikiano ili kuinua uzalishaji wa mazao na mifugo na kuimarisha usalama wa chakula.
Rais Samia amesema mazungumzo yao yalijikita katika namna ya kutumia teknolojia za kisasa za umwagiliaji na ufugaji ili kuongeza tija, huku yakifungua fursa mpya za uwekezaji katika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa nchi.
Ameeleza kuwa bara la Afrika bado linatumia fedha nyingi kuagiza chakula kutoka nje, jambo linalosisitiza umuhimu wa kuongeza uzalishaji wa ndani kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuwekeza katika kilimo chenye tija.
Aidha, Rais Samia amesema Tanzania ina zaidi ya hekta milioni 29 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, hali inayoweka mazingira mazuri kwa uwekezaji mkubwa katika uzalishaji wa chakula kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.
Katika hatua nyingine, amesema Serikali ya Misri imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania kuendeleza Ranchi ya Ruvu, ambayo kwa sasa haijatumika kikamilifu, kwa lengo la kuifanya kuwa kitovu cha uzalishaji wa kisasa wa mifugo na uwekezaji wa pamoja.
Rais Samia pia amewahamasisha wawekezaji kutoka Misri kushirikiana na taasisi za Serikali zenye maeneo makubwa ya uzalishaji, ikiwemo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Magereza, Shirika la Taifa la Ranchi (NARCO), pamoja na miradi ya kilimo inayotekelezwa Zanzibar.
Amesisitiza kuwa ushirikiano huo unalenga kuongeza uzalishaji wa chakula, kuvutia uwekezaji, kuzalisha ajira kwa Watanzania na kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji wa mazao na mifugo kwa soko la Afrika na masoko mengine ya kimataifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...