Na.Mwandishi Wetu-Babati, ManyaraMamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini imeendesha semina ya kuwajengea uwezo Maafisa wa Huduma kwa Wateja, Mahusiano na Sheria kutoka TANESCO na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Kanda ya Kaskazini kuhusu huduma kwa wateja na uzingatiaji wa matakwa ya kisheria.
Akifungua semina hiyo katika Hoteli ya White Rose, Babati, Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, Bw. George Mhina, aliwasisitiza washiriki kuyafahamu vyema majukumu yao ili waweze kutoa majibu sahihi, ya wakati na yanayozingatia sheria, hivyo kuboresha huduma kwa wateja.
Kwa niaba ya washiriki, Bi. Devotha Mayala kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga na Bw. Samwel Mandari kutoka TANESCO waliishukuru EWURA kwa mafunzo hayo, wakieleza kuwa yamewaongezea uelewa na uwezo wa kuwahudumia wateja kwa weledi zaidi.
Semina hiyo ni sehemu ya juhudi za EWURA za kuimarisha uwezo wa watoa huduma na kulinda haki za watumiaji wa huduma za nishati na maji kupitia Udhibiti wa Haki kwa Matokeo Chanya.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...