Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dodoma, Joseph Chitinka, ameviagiza Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) pamoja na Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Dodoma (DORECU) kuandaa mpango kabambe wa ununuzi wa mbegu bora za ufuta ifikapo Agosti 5, 2026, ili kuongeza ushindani wa mazao ya wakulima katika soko la kimataifa.
Akizungumza Julai 30, 2026, wakati wa kufunga mafunzo maalum ya siku tatu kwa viongozi wa AMCOS, wajumbe wa bodi na viongozi wa DORECU jijini Dodoma, Chitinka alisema Mkoa wa Dodoma umejipanga kuhamasisha uzalishaji wa ufuta mweupe wenye thamani kubwa sokoni badala ya kuendelea kutegemea aina za ufuta wa rangi zinazolimwa kwa wingi hivi sasa.
Aidha, aliwataka viongozi wa vyama vya ushirika kuhakikisha matumizi yote ya fedha yanaidhinishwa na maafisa ushirika pamoja na Ofisi ya Mrajisi, huku mikataba yote ya watoa huduma ikifuata taratibu za kisheria ili kuzuia vitendo vya udanganyifu na ubadhirifu wa fedha za wanachama.
Chitinka amesisitiza umuhimu wa kufuata sheria za manunuzi, kuandaa mipango ya kimkakati na kuhakikisha AMCOS zinafanya kazi mwaka mzima badala ya kuwa vyama vya msimu, amewahimiza viongozi kushirikiana na jamii kuongeza wanachama, kuimarisha uzalishaji wa mazao na kutumia kikamilifu mfumo wa stakabadhi za ghala.
Kuhusu uchaguzi wa viongozi wa ushirika, alisema ni wakati wa kutoa nafasi kwa viongozi wapya wenye sifa na kuacha mfumo wa viongozi kukaa madarakani kwa muda mrefu, ameeleza kuwa mchakato wa uchaguzi utaanza mwezi Agosti baada ya maadhimisho ya Nanenane.
Kwa upande wa usimamizi wa fedha, amesema matumizi yote ya fedha za mfumo wa stakabadhi za ghala yatapaswa kupitishwa kwenye bajeti za mwaka ili kuondoa mianya ya matumizi mabaya, amevitaka vyama vilivyoshiriki minada msimu uliopita kuhakikisha vinalipa tozo zote zinazodaiwa kwa wakati.
Naye Mrajisi Msaidizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Richard Izengo, amesema mafunzo hayo yamelenga kuimarisha usimamizi, ukaguzi na uwajibikaji wa vyama vya ushirika, amesisitiza umuhimu wa kuandaa hesabu na kuziwasilisha kwa mkaguzi wa nje ili kuongeza uwazi kwa wanachama.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa DORECU, David Mtimbi Mwaka, amesema mfumo wa stakabadhi za ghala Una matarajio ya mafanikio makubwa zaidi katika misimu ijayo, kufuatia kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti madalali wa mazao Mkoani Dodoma.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...