Bagamoyo imeandika historia mpya baada ya Mashindano ya Mkali wa Chapati Bagamoyo yaliyofanyika tarehe 9 Julai 2026 kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, yakivutia maelfu ya wananchi pamoja na washiriki 170 waliojitokeza kuonesha umahiri wao katika utengenezaji wa chapati.

Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mhe. Mariam Abdallah Ibrahim, huku mwenyeji akiwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. CPA Subira Khamis Mgalu.

Tukio hilo limepongezwa na wananchi kwa kuwa limeleta burudani, limehamasisha vipaji, na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia. Aidha, limeunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mariam Abdallah Ibrahim aliwapongeza washiriki wote 170 kwa kujitokeza na kushiriki kwa ari kubwa, akieleza kuwa kila mshiriki ni mshindi kwa kuthubutu kuonesha kipaji chake. Pia aliwashukuru wananchi wa Bagamoyo kwa mwitikio mkubwa ulioifanya hafla hiyo kuwa ya kipekee na yenye mafanikio makubwa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. CPA Subira Khamis Mgalu, alimpongeza mdhamini wa mashindano hayo, Mhe. Mariam Abdallah Ibrahim, kwa kuandaa tukio hilo muhimu. Alisema mashindano hayo yameimarisha ushirikiano kati ya viongozi na wananchi, huku yakionesha dhamira ya kuendelea kuwaletea wananchi programu zenye manufaa ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.



































Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...