Na Karama Kenyunko - Michuzi Tv
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua rasmi dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027, huku ikiwataka waombaji kufuata taratibu rasmi na kujiepusha na matapeli wanaojifanya mawakala wa udahili.
Dirisha hilo limefunguliwa leo Julai 10, 2026 na litabaki wazi hadi Agosti 10, 2026, ambapo waombaji wote wenye sifa wanatakiwa kuwasilisha maombi yao moja kwa moja kwenye vyuo walivyochagua kupitia mifumo ya kielektroniki ya vyuo husika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 10, 2026 Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa, amesema makundi yanayostahili kuomba udahili ni wenye sifa za Kidato cha Sita, wenye Stashahada (Diploma) au sifa linganifu, pamoja na wenye Cheti cha Awali (Foundation Certificate) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Kihampa amesema waombaji wanapaswa kusoma kwa makini Mwongozo wa Udahili wa Shahada ya Kwanza wa mwaka 2026/2027 unaopatikana katika tovuti ya TCU ili kujua sifa za kujiunga, programu zinazotolewa na vyuo vilivyoidhinishwa pamoja na masharti mengine ya udahili.
Aidha, waombaji wametakiwa kutembelea tovuti za vyuo wanavyotarajia kujiunga navyo ili kupata maelezo ya kina kuhusu programu za masomo, vigezo vya udahili na namna ya kutuma maombi.
Waombaji watanzania wenye vyeti vilivyotolewa nje ya nchi, TCU imeelekeza kuwa ni lazima wapate ithibati ya ulinganifu wa vyeti vyao kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa vyeti vya elimu ya sekondari au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa vyeti vya stashahada kabla ya kutuma maombi.
Kwa upande wa waombaji wasiokuwa Watanzania wenye vyeti vya nje, wameelekezwa kuwasilisha maombi yao moja kwa moja kupitia mifumo ya vyuo husika.
Aidha Kihampa amewahimiza waombaji kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia tovuti ya Tume, tovuti za vyuo vinavyodahili wanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kupitia taarifa rasmi zinazotolewa na Tume.
Wakati huo huo, Tume imetoa tahadhari kwa waombaji na wananchi kwa ujumla kujihadhari na matapeli wanaojitambulisha kuwa mawakala au washauri wa udahili, ikisisitiza kuwa huduma zote za udahili zinapatikana moja kwa moja kupitia vyuo husika.
TCU imeeleza kuwa waombaji wanaohitaji ufafanuzi kuhusu udahili wanapaswa kuwasiliana moja kwa moja na vyuo walivyochagua, huku maswali ya jumla yakitumwa kupitia barua pepe ya Tume.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...