MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) imeendelea na jitihada zake za kuhakikisha upatikanaji wa maji katika kata ya Marangu Mashariki wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro unakuwa ni wa uhakika ambapo wameendelea kuboresha miundombinu kwa kununua mabomba mapya ya kulaza umbali wa kilomita 13.

Akizungumza mara baada ya kuwasili kwa mabomba hayo, Mkuu wa Idara ya Ufundi, Mhandisi Innocent Lugodisha alisema kuwa, mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo mamlaka tayari imeshakamilisha awamu ya kwanza ya mradi.

Mhandisi Lugodisha alisema kuwa, mradi huo unatarajiwa kugharimu shilingi 1,470,121,709 ambapo awamu ya kwanza 234,355,900 na awamu ya pili utatumia 1,235,765,808.

"Mradi huu ukikamilika utasaidia upatikanaji wa maji katika vijiji vya Samanga, Rauya na Ashira kuwa wa uhakika ambapo utaongeza uzalishaji maji kutoka mita za ujazo 402 hadi 4320 kwa siku na mahitaji kwa vijiji hivi ni mita za ujazo 1164" alisema Mhandisi Lugodisha.

Alisema kuwa, awamu ya kwanza ulihusisha ujenzi wa chanzo cha Lyasongoro na Kyerio, ujenzi wa uzio katika chanzo, ujenzi wa break pressure na ulazaji wa bomba zenye urefu wa kilomita 2.4.

Aliongeza kuwa, katika awamu ya pili kazi zitakazoenda kufanyika ni uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba lenye kipenyo cha inchi 8 na 6 lenye urefu wa kilomita 13.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Enock Koola alisema kuwa, mradi huo utakapokamilika utasaidia kuondoa tatizo la maji kabisa katika vijiji vya Rauya, Samanga na Ashira ambavyo vilikuwa vikipata maji chini ya asilimia 50.

"Wakati wa ziara ya Waziri Mkuu mkoani Kilimanjaro niliwasilisha changamoto ya upatikanaji maji katika jimbo letu hususani kata hii ya Marangu mashariki na Waziri Mkuu alimwagiza Waziri wa maji kuhakikisha upatikanani maji kwa wananchi unatatuliwa na aliahidi kulitatua ndani ya muda mfupi na matokeo yameanza kuonekana kupitia mradi huo" alisema Koola.







Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...