Na Victor  Masangu,Bagamoyo 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya  ya Wazazi Taifa Ndg. Fadhili Maganya amekemea vikali baadhi  viongozi wa CCM  wakiwemo madiwani na wabunge kuachana na vitendo vya kupanga safu hasa katika kuelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2027.

Hayo ameyabainisha  wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza kukiimarisha chama pamoja na jumuiya zake zote ikiwa samba samba na kuangalia uhai wa chama.

"Kitu kikubwa ninachowaomba viongozi,madiwani pamoja na wabunge  kuondokana kabisa na masuala ya kuamua kupanga safu kabla ya uchaguzi lkn kitu kikubwa wanaotaka kugombea ruksa kugombea nafasi mbali mbali,"amesema Mwenyekiti huyo.

Pia amefafanua kwamba mwakani ni kipindi cha uchaguzi hivyo hakusita kuwaasa wanachama wote kuanzia ngazi za mashina wasisite kujitokeza katika kugombea nafasi mbali mbali.

Kadhalika ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Kisarawe kwa kuweza kusimamia vizuri utekelezaji wa ilani na ukusanyaji wa fedha za mapato ya ndani ambazo zimekwenda kutekeleza miradi ya maendeleo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amesema kuwa hali ya  mwenendo  katika utekelezaji wa  miradi ya maendeleo inakwenda vizuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Nasri Ally amebainisha kuwa wameweza kufanikisha kukusanya mapato ya ndani kwa asilimi 113 na kuongeza  wana miradi 9 ya kimkakati ikiwemo mradi wa ujenzi wa ya kisasa.

Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe Halfan Sika amebainisha kwamba  wameweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwa sambamba na kushirikiana na serikali katika miradi mbali mbali.

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Kisarawe Selemani Jafo amempongeza Mwenyekiti wa  Taifa kwa kufanya ziara hiyo ya kikazi ambayo itaweza kuleta tija katika maendekeo kwa wananchi.

Mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Pwani Jackson  KItuka amewahimiza viongozi kuhakikisha wanapambana na winbi la baadhi ya matapeli wa ardhi kwani wamekuwa wakisababisha migogoro  ya ardhi. 

Akiwa Wilayani Mkuranga ameridhishwa na uchapa kazi wa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga kwa kuweza kusimamia vema utekelezaji wa miradi mbali mbali.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya CCM Taifa ameendelea na ziara yake ya kikazi  katika Wilaya za Kisarawe pamoja na Wilaya ya mkuranga ambapo ametembelea miradi ya maendeleo ukiwemo Hospitali ya Kisarawe,daraja la Kisopwa,shule ya msingi sanze na chuo cha Veta mkuranga.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...