Na Janeth Raphael - MichuziTv
Benki ya Ushirika Tanzania (COOP Bank Tanzania) imefanya Mkutano Mkuu wake wa Pili tangu kuanzishwa kwake, ambapo viongozi na wanahisa walipokea taarifa ya mafanikio makubwa ya utendaji wa benki hiyo katika kipindi cha miaka miwili, yakionyesha ukuaji wa kasi katika sekta ya benki nchini.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa COOP Bank Tanzania, Godfrey Ng'urah, amesema mkutano huo umekuwa fursa ya kutafakari safari ya mageuzi ya benki hiyo na hatua mbalimbali zilizofikiwa tangu kuanzishwa kwake.
Amesema mafanikio hayo yametokana na uongozi uliojikita katika mabadiliko, ambao umewezesha benki kuongeza kwa kiwango kikubwa rasilimali, wafanyakazi, matawi pamoja na ukubwa wa mizania ya benki ndani ya muda mfupi.
Ng'urah amesema viashiria vya utendaji vinaonesha kuwa COOP Bank ndiyo benki inayokua kwa kasi zaidi nchini kwa sasa, huku ikishuhudia ongezeko kubwa la wafanyakazi, upanuzi wa mtandao wa matawi na kuimarika kwa huduma zinazowafikia wateja katika maeneo mbalimbali.
Kwa upande wa utoaji wa mikopo, alisema benki imeendelea kuwawezesha wanachama wa vyama vya ushirika, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara pamoja na taasisi mbalimbali za ushirika, ambapo kitabu cha mikopo kimeongezeka kutoka Sh bilioni 14 mwaka 2024 hadi kufikia Sh bilioni 102 mwaka 2025.
Aidha, amesema amana za wateja zimeongezeka kutoka Sh bilioni 15 hadi kufikia Sh bilioni 114 mwishoni mwa mwaka wa fedha uliopita, huku mtaji wa wanahisa ukikua kutoka Sh bilioni 27 hadi Sh bilioni 42, jambo linaloonyesha kuimarika kwa msingi wa kifedha wa benki hiyo.
Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa COOP Bank imeendelea kupanua wigo wa bidhaa na huduma zake bunifu kwa kuanzisha akaunti nafuu zinazorahisisha uwekaji wa amana pamoja na kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali inayowawezesha wateja kupata huduma kwa urahisi zaidi.
Ameongeza kuwa benki hiyo imezindua huduma ya COOP PESA, mfumo wa kisasa wa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi unaowawezesha wateja kufanya miamala mbalimbali kwa urahisi, usalama na wakati wowote bila kulazimika kufika tawi.
Ng'urah amesema COOP Bank itaendelea kuwekeza katika ubunifu wa huduma za kifedha na teknolojia ili kuongeza ujumuishi wa kifedha, kuwafikia Watanzania wengi zaidi na kuchochea maendeleo ya sekta ya ushirika pamoja na uchumi wa nchi kwa ujumla.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...