Skauti Mkuu wa Tanzania, Lt. Rashid Mchata, amesema ushirikiano kati ya Chama cha Skauti Tanzania (Tanzania Scouts Association-TSA) na Oryx Gas Tanzania Limited ni hatua ya kimkakati itakayowawezesha maelfu ya vijana wa Skauti na Watanzania kwa ujumla kupata maarifa, ujuzi na fursa za kushiriki katika maendeleo ya Taifa kupitia matumizi salama ya nishati safi.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano huo leo Jumatano Julai 15, 2026, Lt. Mchata amesema hafla hiyo si tukio la kawaida la kusaini hati, bali ni tamko la dhamira, daraja la fursa na mwanzo wa safari ya pamoja ya kuwaletea vijana mabadiliko chanya yatakayodumu kwa miaka mingi.
Amesema TSA inaamini kuwa kijana mwenye maarifa ni nguvu ya Taifa, mwenye ujuzi ni rasilimali muhimu ya maendeleo, huku mwenye maadili na nidhamu akiwa msingi wa mustakabali wa Tanzania.
Lt. Mchata ameeleza kuwa kupitia makubaliano hayo, Skauti Tanzania itaunganisha mtandao wake mkubwa wa vijana na utaalamu wa Oryx Gas Tanzania katika sekta ya gesi ya LPG ili kuimarisha elimu ya matumizi salama ya nishati safi, usalama wa jamii, maandalizi ya kukabiliana na dharura pamoja na kuwaongezea vijana ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kupata ajira.
Amesisitiza kuwa, lengo si kuwaeleza vijana kuhusu fursa zilizopo pekee, bali kuwajengea uwezo wa kuzitambua, kuzitumia na kuzalisha fursa mpya zinazochochea maendeleo ya Taifa.
Aidha, amesema TSA itasimamia utekelezaji wa ushirikiano huo kwa uwajibikaji mkubwa ili kuhakikisha unaleta matokeo yaliyokusudiwa, huku akiwataka vijana wa Skauti kutumia nafasi hiyo kujifunza, kujenga uwezo na kuwa wabunifu katika kulitumikia Taifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Energies Tanzania, Benoit Araman, amesema kampuni hiyo imeamua kushirikiana na Skauti baada ya kuona kuwa harakati zao zina misingi inayolingana na malengo ya Oryx ya kuitumikia jamii kupitia elimu ya matumizi salama ya gesi ya LPG.
Amesema dhima ya Skauti ya kuwa tayari wakati wote kuhudumia jamii ndiyo iliyowafanya kuitambua TSA kama mshirika sahihi wa kutekeleza programu ya utoaji elimu kuhusu matumizi salama ya gesi kwa wananchi.
Araman ameongeza kwa kusema kuwa, Oryx kwa kushirikiana na wataalamu wake itatoa mafunzo kwa wawakilishi wa Skauti kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambao baadaye watakuwa wakufunzi na mabalozi wa kuielimisha jamii namna sahihi ya kutumia gesi ya LPG kwa usalama.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu matumizi salama ya nishati safi, kupunguza ajali zinazotokana na matumizi yasiyo sahihi ya gesi na kuchangia ustawi wa jamii kwa muda mrefu.
Naye Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, Abubakari Mtitu, amesema, mkataba huo ni sehemu ya mkakati endelevu wa kuhakikisha vijana wanapata mafunzo ya weledi kuhusu matumizi ya nishati safi na tahadhari zinazopaswa kuzingatiwa wakati wa matumizi yake.
Ameendelea kwa kusema kuwa, ushirikiano huo unaendana na misingi ya Skauti ya kutekeleza wajibu kwa Mungu, kwa wengine na kwa nafsi binafsi, huku ukiwapa vijana nafasi ya kutumia elimu watakayopata kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.
Mtitu amesema kupitia mafunzo hayo, vijana wa Skauti pamoja na vijana wengine wa Tanzania watawezeshwa kuwa mabalozi wa matumizi salama ya nishati safi, hatua itakayochangia kujenga jamii salama na kuifanya dunia kuwa mahali bora zaidi kuliko walivyoikuta.
Ameongeza kwa kusema kuwa, TSA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuandaa programu zinazowajengea vijana uwezo, maadili na ujuzi unaohitajika katika kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...