Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, Oryx Gas Tanzania imetoa mafunzo ya matumizi salama na sahihi ya gesi ya kupikia kwa makundi ya wajasiriamali mbalimbali yakiwemo mama na baba lishe.

Mafunzo hayo yametolewa leo Julai 23,2026 katika Tamasha la Samaki Bagamoyo ambapo wajasiriamali zaidi ya 600 ambao wanashiriki tamasha hilo wamepatiwa mafunzo hayo kupitia maofisa wa Oryx Gas wakiongozwa na Meneja Mafunzo Peter Ndomba.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Ndomba ametumia nafasi hiyo kuelezea amesema faida za kutumia LPG ikilinganishwa na nishati nyingine za kupikia, ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji, kuokoa muda wa kupika, kulinda afya kwa kupunguza moshi hatarishi, na kuhifadhi mazingira.

Pia amesema wajasiriamali na washiriki wa tamasha hilo wamejifunza mbinu bora za usalama zikiwemo ukaguzi wa mtungi, regulator na bomba kabla ya matumizi.

Nyingine ni namna ya kutambua uvujaji wa gesi na hatua sahihi za kuchukua,matumizi ya vifaa vilivyoidhinishwa na vyenye ubora,uhifadhi salama wa mitungi ya gesi, tahadhari za kuzuia ajali na hatua za kuchukua wakati wa dharura.

Aidha wamefundishwa mbinu bora za matumizi salama ya LPG katika shughuli za kila siku za upishi pamoja na athari za kuni na mkaa kwa mazingira na afya ya jamii hasa kwa kundi kubwa la wanawake ambao wanaathirika wa moshi wa kuni na mkaa kila siku.

“Kupitia mafunzo haya, Oryx Gas Tanzania inaendelea kuwawezesha wafanyabiashara wa chakula kutumia nishati safi kwa usalama, kuongeza ufanisi wa biashara zao na kuchangia afya bora pamoja na mazingira safi.

“Elimu ya matumizi salama ya LPG ni msingi wa kujenga jamii salama na kufanikisha ajenda ya taifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.Oryx Gas Tanzania imekuwa kinara wa nishati safi na sasa imejikita pia kutoa elimu kwa makundi mchini Tanzaia ili kuhakikisha matumizi endelevu ya nishati safi.”










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...