Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) inaendelea kuimarisha uzalishaji na biashara ya zao la kitunguu kwa kukamilisha miongozo ya usimamizi wa zao hilo na kuendeleza miundombinu ya masoko, hatua zinazolenga kuongeza ushindani wa vitunguu vya Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi Wilaya ya Karatu, Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb), ameielekeza COPRA kukamilisha miongozo ya zao la kitunguu ndani ya miezi mitatu na kuanza mchakato wa kupanua Soko la Vitunguu la Endashangwet ili kuongeza fursa za masoko kwa wakulima.

Akipokea maelekezo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi. Irene Mlola, amesema miongozo hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilishwa na itaweka mfumo rasmi wa biashara ya vitunguu kupitia matumizi ya vipimo sahihi, vifungashio sanifu na usimamizi bora wa masoko.

Katika mwaka 2025/2026, Tanzania ilisafirisha kilogramu *33,295,659* za vitunguu zenye thamani ya zaidi ya *Shilingi bilioni 1.9*. Kupitia hatua hizi, Serikali inalenga kuongeza thamani ya zao, kupanua masoko ya kimataifa na kuongeza kipato cha wakulima. 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...