Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Rabia Abdalla Hamid, ametembelea wanufaika wa mikopo ya halmashauri kwa makundi maalum mkoa wa Mbeya.
Akizungumza alipotembelea na kukagua miradi hiyo wakati wa kusikiliza makundi ya kijamii Mkoa wa Mbeya, Rabia aliwataka wanufaika wa mikopo hiyo kurejesha kwa wakati ili kuweza kuendelea kunufaisha na wengine.
"Nimeridhishwa na vikundi hivi vya Samaki na kiwanda kidogo cha Fanicha, ni miradi mizuri na inamanufaa kwa wanufaika wa Mikopo hii na jamii kwa ujumla. Inaridhisha na ina onyesha uwezako mkubwa wakurejesha ," alisema.
Aidha ndugu Rabia amesema Serikali chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan itaendelea kutatua na kuhakikisha upatikanaji wa Mikopo kwa makundi yote stahiki, amezitaka Halmashauri kuendelea kuongeza Kasi ya Utoaji wa mikopo hiyo kwa wale wenye sifa stahiki.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...