Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua rasmi huduma za usafiri wa umma kwa kutumia mabasi ya umeme pamoja na Kituo cha Mabasi Malindi leo, tarehe 23 Julai 2026.

Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi ameitaka ZSSF kukamilisha kwa haraka ujenzi wa vituo vya kisasa vya mabasi ili wananchi wanufaike kikamilifu na huduma hiyo. Amesema mradi wa mabasi ya umeme utaboresha usafiri wa umma, kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuongeza matumizi ya nishati safi.

Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi  amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo barabara, maji, bandari, viwanja vya ndege, hospitali na Mji wa Michezo unaojiandaa kuhudumia mashindano ya AFCON, huku akiwataka wananchi kuilinda miundombinu ya umma na kuendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo.

Hafla hiyo pia ilihusisha uzinduzi wa kadi maalumu za usafiri kwa wanafunzi, wazee na abiria wengine, hatua inayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za usafiri kwa makundi mbalimbali ya wananchi.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...