Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maji ili kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika mikoa yote ya Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 15 Julai 2026, Ikulu Zanzibar, alipokutana na Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Nadir Abdullatif, pamoja na Waziri wa Maji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jumaa Aweso.

Amesema miradi ya maji tayari imeanza kuleta matokeo katika mikoa ya Kaskazini Unguja, Kusini Unguja na Mjini Magharibi, huku akisisitiza matumizi ya teknolojia za kisasa na kuimarisha ushirikiano kati ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za maji.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jumaa Aweso, ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa miradi ya maji na kueleza kuwa wizara yake imeandaa mfumo wa kidijitali utakaowezesha wananchi kutoa taarifa za changamoto za huduma ya maji ili zipatiwe ufumbuzi kwa haraka.

Vilevile, amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...