Jane Mwakyoma, July 15, 2026, Rukwa.

MKUU wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa kufanikiwa kupata hati safi akieleza kuwa mafanikio hayo ni kielelezo cha usimamizi bora wa fedha za umma na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Nyerere ametoa pongezi wakati akizungumza katika Baraza Maalum la Madiwani la kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Amesema mafanikio hayo yametokana na ufungaji mzuri wa vitabu vya hesabu za Serikali, uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za umma, usimamizi madhubuti wa rasilimali, ukusanyaji mzuri wa mapato, utekelezaji wa bajeti kwa ufanisi, pamoja na ushirikiano imara kati ya Menejimenti ya Halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Aidha amesisitiza kuwa mafanikio hayo yanaendelea kuimarisha uwajibikaji, uwazi na usimamizi bora wa rasilimali za umma kwa manufaa ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

Pia ameitaka Halmashauri kuendeleza juhudi hizo ili kudumisha viwango vya utendaji na utoaji bora wa huduma kwa wananchi.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...