Rais wa IPU afuata nyayo za kiongozi mashuhuri wa Afrika katika ziara yake rasmi ya kikazi nchini Burkina Faso, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson ametembelea na kujionea Kituo cha Kumbukumbu cha Thomas Sankara akiambatana na Naibu Spika wa Bunge la Burkina Faso Mhe. Haoua Fofana pamoja na wajumbe wa wabunge.

Wakati wa ziara hiyo, Rais wa IPU ametembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho na kuona alama zinazoakisi safari, misingi ya mawazo na dhamira ya Kapteni Thomas Sankara katika kuwakomboa watu wake na bara la Afrika.

Waongoza wageni wametoa maelezo ya kina kuhusu hatua muhimu za maisha ya Thomas Sankara mazingira yaliyochochea harakati zake za kisiasa na athari endelevu za urithi wake, maelezo hayo yameupa wajumbe hao uelewa mpana zaidi wa historia inayomzunguka shujaa huyo wa Burkina Faso.

Akiwa ameguswa sana kihisia, Dkt. Tulia Ackson ameeleza kuwa ni heshima kubwa kuwepo katika eneo lenye historia nzito na muhimu, amebainisha kuwa ingawa historia ya Thomas Sankara inajulikana sana kupitia vitabu, majarida na vyombo vya habari, kuishuhudia ana kwa ana kunaleta hisia za kipekee.

Ziara hii katika kituo cha kumbukumbu cha Thomas Sankara imempa Rais wa IPU Mhe. Dkt. Tulia Ackson uelewa bora zaidi wa nafasi ambayo Kapteni Thomas Sankara anaendelea kuwa nayo katika kumbukumbu za watu iwe ni nchini Burkina Faso au kimataifa.









Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...