Na Janeth Raphael - MichuziTv
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Misri zimefikia makubaliano ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya usafirishaji wa baharini kwa kuunganisha bandari za mataifa hayo mawili, hatua inayolenga kuongeza biashara, kuvutia uwekezaji na kupanua masoko ndani ya Afrika na ukanda wa Ghuba.
Akizungumza Ikulu, Dar es Salaam, Julai 18, 2026, baada ya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi, Rais Samia alisema ushirikiano huo utahusisha maendeleo ya Bandari ya Dar es Salaam pamoja na ujenzi wa eneo maalumu la kuhifadhi bidhaa na makontena ya Misri katika Bandari ya Bagamoyo, ambalo litaunganishwa na reli hadi Kwala ili kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo.
Amesema pande zote mbili zimekubaliana kuendeleza mazungumzo ya kuunganisha Bandari za Dar es Salaam, Bagamoyo, Safaga pamoja na bandari nyingine za Misri, jambo litakalorahisisha usafirishaji wa bidhaa, kupunguza gharama za biashara na kuongeza ushindani wa mataifa hayo katika soko la kimataifa.
Kwa mujibu wa Rais Samia, mpango huo utafungua njia kwa bidhaa za Tanzania kuingia kwa urahisi zaidi katika masoko ya nchi za Ghuba, huku bidhaa kutoka Misri zikipata fursa ya kufikia nchi za Afrika Mashariki na Kusini kupitia bandari za Tanzania.
Katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, Rais Samia amesema Rais El-Sisi ameambatana na ujumbe wa wafanyabiashara wakubwa 35 wanaoshiriki Jukwaa la Biashara Tanzania na Misri, hatua inayotarajiwa kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya mataifa hayo mawili.
Aidha, amesema Shirika la Ndege la EgyptAir tayari linaendesha safari tatu kwa wiki kati ya Misri na Tanzania, huku akiihimiza Air Tanzania kuanzisha safari za moja kwa moja kuelekea Misri ili kurahisisha usafiri wa abiria, kukuza utalii na kuongeza fursa za biashara.
Rais Samia amesisitiza kuwa ushirikiano huo unaipa Tanzania nafasi ya kuendelea kuwa kitovu muhimu cha biashara na usafirishaji kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, huku ukiimarisha zaidi uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na Misri.

.jpeg)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mikataba na Hati za Makubaliano katika sekta ya umeme, nishati jadidifu, pamoja na masuala ya mbalimbali za Uchukuzi baina ya Tanzania na Misri. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 18 Julai, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo rasmi na Ujumbe wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, uliongozwa na Rais wa nchi hiyo, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 18 Julai Juni, 2026.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...