Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amesema Mkoa wa Iringa unaendelea kujipambanua kama mkoa wenye fursa ya utalii, kilimo, huku akiwakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kufika mkoani humo kutumia fursa zilizopo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Juni 3, 2026, mara baada ya kutembelea banda la Mkoa wa Iringa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Mhe. Kheri amesema Iringa imebarikiwa vivutio vya kipekee vya utalii vinavyoifanya kuwa eneo lenye fursa kubwa za uwekezaji.

Ameitaja Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuwa miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyovutia watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani, akisisitiza kuwa wawekezaji wenye ndoto ya kuwekeza katika sekta ya utalii wanapaswa kuichagua Iringa kutokana na mazingira yake rafiki kwa biashara.

Aidha, ameeleza kuwa Iringa ina maeneo mengi ya kimkakati yanayofaa kwa kilimo cha biashara na ndiyo mkoa unaoongoza nchini kwa kuwa na skimu kubwa za umwagiliaji, hali inayowezesha uzalishaji wa mazao kwa kiwango kikubwa mwaka mzima.

Mhe. Kheri amebainisha kuwa wawekezaji wanaolenga sekta ya mazao, hususan zao la mpunga na shughuli za kuongeza thamani ya mazao ya mbao , wana kila sababu ya kuwekeza Iringa, akieleza kuwa mkoa huo una mazingira yanayowezesha ukuaji wa uwekezaji wenye tija.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...