Na Mwandishi wetu

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema itaendelea kuweka msukumo katika kuendeleza sayansi na teknolojia kwani ndiyo msingi wa kukuza uchumi kupitia maarifa na kuboresha huduma katika sekta mbalimbali.

Akizungumza  Julai 8, 2026, baada ya kutembelea Taasisi ya Afya na Utafiti ya Ifakara (Ifakara Health Institute-IHI), tawi la Bagamoyo mkoani Pwani, Prof. Mkenda amesema taasisi hiyo ni ya mfano katika tafiti za kisayansi ambazo zinasaidia maendeleo ya sekta ya afya.

Amepongeza kazi za Taasisi hiyo akitolea mfano utafiti chanjo za malaria, majaribio ya dawa (clinical trials) na teknolojia za kisasa zinazotumika  katika utafiti.

Mkenda amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa IHI na vyuo vikuu vya ndani na vya kimataifa ili kuijengea Tanzania yenye uwezo wa kufanya tafiti zenye viwango vya kimataifa, kuzalisha maarifa na bidhaa zenye manufaa kwa wananchi.

Prof. Mkenda ameongeza kuwa serikali inataka kuona dawa za asili zikifanyiwa utafiti, majaribio ya awali (pre-clinical) na clinical trials ili kuthibitisha ubora na usalama wake  hapa hapa nchini, hatua itakayowezesha Tanzania kuzalisha dawa zilizotokana na gunduzi za ndani na  kunufaika na matokeo yake  kwa kuwa na haki miliki.

Aidha, amesema wizara inaendelea kupitia sera ya Sayansi na Teknolojia ili kuhakikisha inakuwa shirikishi, inatekelezeka na inapimika, sambamba na kuvitaka vyuo vikuu nchini kuweka uzito sawa katika ufundishaji na utafiti.

Akizungumza kwa niaba ya  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Afya na Utafiti ya Ifakara (Ifakara Health Institute-IHI), tawi la Bagamoyo Dkt Ally Olotu amesema taasisi hiyo immejikita katika kuleta mabadiliko katika mifumo ya afya nchini na nje ya mipaka, kufanya tafiti za chanjo mbalimbali na tabia za jamii kuhusiana na Afya. 









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...