UBINGWA wa kuwania Taji hili la Dunia umezidi kunoga kwenye hatua hizi za mtoano kwani kila timu inazidi kupambana kuvuka kwenye hatua inayofuata. Lakini na wewe unaweza ukapiga pesa mechi za leo, hivyo ingia na ubashiri hapa.
Australia vs Misri huu ni mchezo ambao timu zote mbili unaihataji na ambao utakuwa na ushindani mkubwa kabisa kwani wote wawili wanapambania nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora kwenye michuano hii mikubwa.
Misri kutoka Bara la Afrika ni moja ya timu ambayo inatarajiwa kufanya vizuri kwenye michuano hii mikubwa kwani kwenye Kundi G ambalo alikuwa aliweza kumaliza nafasi ya pili akiwa sawa na kinara wa kundi hilo tofauti yao ilikuwa ni magoli ya kufungwa na kufunga pekee.
Timu hii ambayo inaongozwa na nahodha wao Mohamed Salah wanatarajia kuwafunga Australia ambao wao walimaliza nafasi ya pili nao katika Kundi D baada ya kukusanya pointi 4. Timu hizi kwenye viwango vya FIFA hazijatofautiana sana kwani mpaka sasa yoyote anaweza akaondoka na ushindi.
Pesa ipo leo kwenye michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile Keno, Aviator, Poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Australia nguvu ya timu yao ipo kwenye umoja wa timu na utekelezaji wa maelekezo ya kocha. Wanapenda kushambulia kupitia pembeni na kutumia mipira ya juu, jambo linaloweza kuwasumbua mabeki wa Misri ikiwa hawatakuwa makini.
Huku Misri wao wanaingia wakiwa na mtindo tofauti kabisa. Mafarao wanategemea zaidi utulivu, umiliki wa mpira na ubunifu wa viungo wao kutengeneza nafasi za kufunga.
Pia wana uwezo mkubwa wa kushambulia kwa kasi wanapopata nafasi za mashambulizi ya kushtukiza. Ikiwa watafanikiwa kuhimili presha ya Australia na kucheza kwa utulivu, wana uwezo wa kuumiza wapinzani wao kwa pasi za haraka na umaliziaji mzuri. Jisajili hapa na ubashiri mechi hii.
Lakini jambo jingine litakaloweza kuamua matokeo ni uwezo wa kila timu kutumia nafasi chache zitakazopatikana. Katika hatua ya mtoano, mara nyingi timu inayotumia nafasi yake ya kwanza vizuri ndiyo huondoka na ushindi. Aidha, benchi la ufundi na mabadiliko ya wachezaji kipindi cha pili yanaweza kubadilisha kabisa mwelekeo wa mchezo.
Hivyo mchezo huu una kila dalili za kuwa mgumu na wenye tahadhari nyingi, huku timu zote zikiepuka kufanya makosa ya kizembe. Endapo kutakuwa na mshindi ndani ya dakika 90, kuna uwezekano ushindi huo ukapatikana kwa tofauti ya bao moja pekee. Pia si jambo la kushangaza kama mchezo utaenda hadi muda wa nyongeza au hata mikwaju ya penalti.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...