
SERIKALI imewaahidi wakazi wa kijiji cha Endashangwet, Wilayani Karatu katika Mkoa wa Arusha kuwa ujenzi wa soko la vitunguu ukikamilika kwa awamu zote litakuwa soko la kuuza vitunguu masoko ya kimataifa zaidi ya soko la Kenya.
Ametoa ahadi hiyo Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) akiwa ziarani Arusha kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025–2030, tarehe 22 Julai 2026, ambapo ameambatana na Viongozi mbalimbali wa Serikali kutatua kero za wananchi kama mlezi wa Mkoa huo.
“Nimepokea ombi la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha (CCM), Mhe. Cecilia Pareso la kupanua ukubwa wa soko hili. Naielekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kuhakikisha inaanza mchakato wa kupanua ujenzi wa soko, huku ikitafuta masoko mengine ya vitunguu nje ya nchi. Dhamira ya Serikali ni kuona wakulima wa vitunguu katika Wilaya ya Karatu sasa wanakuwa na soko la kuuza vitunguu wanavyozalisha kimataifa kutokana na ubora wake,” amesema Mhe. Daniel Chongolo.
Awamu ya kwanza ya ujenzi wa soko la kijiji cha Endashangwet lenye gharama ya Shilingi Milioni 500 imepangwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu, ambapo Waziri Chongolo amesisitiza ubora wa miundombinu katika ujenzi huo uzingatiwe.
Wilaya ya Karatu imejikita na shughuli mbalimbali za maendeleo wakiwemo wakulima wanaolima mazao ya vitunguu, ngano, mbaazi, mahindi na maharage


.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...