Na Said Mwishehe,Michuzi TV
SERIKALI imeanzisha Chama cha Wahandisi wa Nishati (Association of Energy Engineers - AEE) Tanzania Chapter, hatua inayolenga kuimarisha ufanisi wa matumizi ya nishati, kupunguza upotevu wa umeme na kusaidia ukuaji endelevu wa sekta ya viwanda.
Chama hicho kilichoanzishwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), kitaongoza juhudi za kukabiliana na upotevu wa nishati unaokadiriwa kufikia asilimia 10 hadi 15, huku kikihamasisha matumizi bora ya nishati katika viwanda, taasisi na majengo ya biashara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi jijini Dar es Salaam leo Julai 31,2026, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira wa Wizara ya Nishati, Emilian Nyanda, alisema Tanzania imeweka sera na mikakati mbalimbali ya kuboresha ufanisi wa matumizi ya nishati, lakini mafanikio yake yanategemea uwepo wa wataalamu wenye ujuzi.
“Bila kuwa na wataalamu wa kutosha, itakuwa vigumu kufikia malengo ya taifa ya kuongeza ufanisi wa matumizi ya nishati,” alisema Nyanda.
Alisema utekelezaji wa Mpango Kazi wa Ufanisi wa Nishati umewezesha kuzalishwa kwa wakaguzi wa nishati 60 wenye ithibati, watakaosaidia kufuatilia matumizi ya nishati na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho.
Nyanda alisema wataalamu hao watafanya ukaguzi katika viwanda, majengo ya biashara na taasisi za umma ili kubaini njia za kupunguza matumizi ya nishati bila kuathiri uzalishaji au utoaji wa huduma.
Alisema matumizi bora ya nishati yatasaidia kupunguza gharama za uzalishaji, hasa katika viwanda ambako umeme ni sehemu kubwa ya gharama za uendeshaji, hivyo kuongeza ushindani wa bidhaa zinazozalishwa nchini.
Aliongeza kuwa chama hicho kitatoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali kuhusu sera na mikakati ya nishati, huku kikihamasisha matumizi yenye uwajibikaji na kupunguza upotevu usio wa lazima.
Nyanda alisema kupunguza upotevu wa nishati kutapunguza pia shinikizo la uwekezaji katika miradi mipya ya umeme kwa kuhakikisha nishati inayozalishwa, ikiwemo kutoka Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere, inatumika kwa ufanisi.
Meneja wa Maendeleo ya Vipaji wa UNDP, Veronica Sigalla, alisema AEE Tanzania Chapter inapaswa kuwa jumuishi kwa kutoa fursa kwa vijana, wanawake, wahandisi, mafundi, watafiti na wataalamu wa sekta ya nishati.
Alisema UNDP itaendelea kushirikiana na Wizara ya Nishati, Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Ireland na wadau wengine kuimarisha mfumo wa ufanisi wa matumizi ya nishati nchini.
Rais wa AEE Tanzania Chapter, Atupele Kilindu, alisema chama hicho kitakuwa jukwaa la wataalamu wa nishati kuimarisha ujuzi, kubadilishana maarifa, kukuza ubunifu na kuchangia utekelezaji wa malengo ya taifa katika sekta ya nishati.
“Kuanzishwa kwa AEE Tanzania Chapter kunaipa Tanzania jukwaa la kitaaluma litakalowawezesha wataalamu kuendelea kujifunza, kuendeleza ubunifu na kuunga mkono ajenda ya maendeleo endelevu ya nchi,” alisema Kilindu.
Alisema chama hicho kitaweka mkazo katika mafunzo ya kitaaluma, programu za uthibitishaji, utafiti, ubunifu, kulea wataalamu vijana na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za elimu, sekta binafsi na washirika wa maendeleo.

Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira wa Wizara ya Nishati, Emilian Nyanda (wapili kushoto) akizindua tawi la kwanza la Chama cha Wahandisi wa Nishati (Association of Energy Engineers - AEE) nchini, katika hafla iliyofanyoika leo jijini Dar es Salaam, watatu kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Vipaji wa UNDP, Veronica Sigalla, na Rais wa AEE, Tupele Kilindu, katikati.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...