Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha

SERIKALI imeipongeza Menejimenti na uongozi wa chuo cha ufundi Arusha (ATC), kutokana na bunifu mbalimbali zinazoendelea kufanywa chuoni hapo ikiwemo ujenzi wa karakana ya kisasa kwaajili ya kufundishia na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Hussein Mohamed Omar, 24Julai 2026 jijini Arusha katika ziara yake ya kikazi chuoni hapo.

Dkt.Omar amesema ujenzi wa karakana hiyo ya kufundishia (Teaching Industry), utasaidia ongezeko kubwa la udahili wa wanafunzi chuoni hapo pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa wanafunzi watakaopata elimu chuoni hapo.

Amesema Menejimenti ya chuo hicho chini ya Mkuu wake wa chuo Profesa Mussa Chacha pamoja na uongozi wa bodi ya chuo unastahili kupongezwa kwa kuwa umekuwa ukitafsiri sera ya Elimu kwa vitendo.

" Kwa niaba ya Serikali napenda kuwapongeza sana kuwekeza katika Ubunifu, lakini pia kwa kutafsiri sera ya Elimu kwa vitendo, ujenzi wa Karakana hii ni ubunifu wa hali ya juu, utaongeza udahili wa wanafunzi lakini pia kutoa ajira kwa wanafunzi watakaopata Elimu ya ufundi hapa hapa chuoni," amesema na kuongeza:

"Na wanafunzi wengine watakaofaulu vizuri pia wataajiriwa hapa hapa katika Karakana hii kwaajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo zitatumika ndani na nje ya nchi," amesema.

Dkt. Omar amesema kuwa tafsiri ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kutafsiri Sera ya Elimu na maono ya dira ya Taifa ya 2050 ya kuhakikisha watanzania wengi wanapata elimu na Ujuzi wa kujiajiri wenyewe.

"Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kinaendelea kuimarisha elimu ya ufundi nchini kupitia ujenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji (Industrial Workshop), mradi unaolenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa vitendo, uzoefu wa kazi na kuwaandaa kwa soko la ajira," amesema Dkt Omar.

Kupitia kiwanda hicho, wanafunzi watashiriki katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo kuchonga vipuri vya magari, kupata uzoefu wa kazi, kuongeza uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa, na hivyo kujipatia kipato wakati wa masomo.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Prof. Musa Chacha, amesema mradi huo unaunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuzalisha wahitimu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya uchumi wa kisasa.

Amesema chuo chake kimeshaanza uzalishaji wa mita janja zinazotumika kusoma Dira ya maji kwa malipo ya kabla (pre paid bill), hatua inayoonyesha dhamira ya chuo kuunganisha elimu, teknolojia na maendeleo ya viwanda nchini.

Prof. Chacha amesema kiwanda hicho kitatumika pia kufanya uzalishaji wa mita hizo janja ambazo zitasambazwa kwa mamlaka za maji nchini ambazo zitakuwa tayari kuanza kuzitumia.

Meneja msimamizi wa MRADI wa Ujenzi wa kiwanda Cha Kufundishia (Teaching Industry) Mhandisi, Elineema Willium amesema mradi huo umewezeshwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Austria kupitia mkopo wa masharti nafuu.

Mhandisi Msuya amesema kuwa mradi huo umeleta manufaa makubwa kwa wanafunzi chuoni hapo,kwa kuwa wanafunzi wamejifunza Teknolojia mpya kupitia Ujenzi huo kutoka nchini Austria.






Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...