Sajenti wa Polisi (SGT) Noela Pallangyo, kutoka Jeshi la Polisi Nchini Tanzania ambaye kwa sasa anahudumu katika Misheni ya Kulinda Amani nchini Sudan Kusini chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), ametunukiwa Barua ya Pongezi kwa kutambua utendaji wake wa kipekee, weledi na mchango wake katika utekelezaji wa majukumu ya kulinda amani.
Amebainisha kuwa baada ya kupokea pongezi hiyo, SGT Noela ameweka wazi kuwa tuzo hiyo ni heshima kwake binafsi Pamoja na nchi yake na Jeshi la Polisi Tanzania huku akiwashukuru viongozi wake na askari wenzake kwa ushirikiano uliomwezesha , kufikia hatua hiyo ya kutunukiwa Barua hiyo.
Barua hiyo ya pongezi imetolewa kwa kutambua huduma yake ya mfano kwa kazi yake chini ya mwamvuli huo wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), ambapo aliweza pia kutekeleza majukumu yake kama Afisa wa Rasilimali Watu (Personnel Officer) katika Makao Makuu ya Mission Headquarters – (MHQ).
Katika barua hiyo, kutoka Umoja huo (UNMISS) imeeleza kuwa SGT Noela amehudumu kwa umahiri, bidii na weledi wa hali ya juu, huku akionyesha kiwango kikubwa cha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake huku Misheni hiyo pia ikitambua mchango wake na umuhimu katika kufanikisha utekelezaji wa mamlaka ya (UNMISS) ya kulinda amani nchini Sudan Kusini.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...