Dar es Salaam, Julai 3, 2026 

Serikali imekipongeza Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mafanikio makubwa ya kupanua huduma zake nchini, hatua iliyowezesha kuongeza fursa za mafunzo kwa watumishi wa umma na wananchi kupitia ongezeko la kampasi kutoka mbili hadi sita katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Jakaya Kikwete, wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya TPSC yaliyofanyika katika Julius Nyerere International Convention Centre.

"Katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, Chuo hiki kimepitia hatua kubwa za maendeleo. Kutoka kampasi mbili wakati wa kuanzishwa kwake hadi kufikia kampasi sita leo; kutoka programu chache za mafunzo hadi kuwa taasisi inayotoa mafunzo ya muda mfupi, programu za muda mrefu, mafunzo kwa njia ya mtandao, tafiti tumizi na shauri za kitaalamu," alisema Kikwete.

Alisema maendeleo hayo yanaonesha dhamira ya TPSC ya kuhakikisha mafunzo ya utumishi wa umma yanawafikia Watanzania wengi zaidi na kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya Serikali katika kujenga watumishi wenye ujuzi, weledi na maadili.

Mbali na kupanua mtandao wa kampasi, Kikwete alisema Chuo kimeongeza wigo wa programu zake za mafunzo kwa kuanzisha mafunzo ya muda mfupi, muda mrefu na mafunzo kwa njia ya mtandao, sambamba na kuimarisha tafiti tumizi na ushauri wa kitaalamu unaosaidia taasisi za umma kuboresha utendaji wake.

Alibainisha kuwa mafanikio hayo yameifanya TPSC kuwa moja ya taasisi muhimu za Serikali katika kuendeleza rasilimali watu na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa niaba ya Serikali, Kikwete aliwapongeza viongozi wote waliowahi kuongoza Chuo, wafanyakazi wa sasa na wa zamani, Bodi za Ushauri pamoja na wadau mbalimbali kwa mchango wao katika mafanikio hayo, akisema hatua iliyofikiwa ni matokeo ya maono ya uongozi, ushirikiano na uzalendo wa watumishi waliojitolea kuijenga TPSC kuwa taasisi yenye hadhi ya kitaifa na kikanda























 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...