Na Mwandishi Wetu
WANANCHI wanaotembelea Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) wanaendelea kunufaika na huduma mbalimbali za mawasiliano na ofa maalum zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kupitia banda lake lililopo katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere.

Katika banda hilo, maafisa wa TTCL wanatoa elimu kuhusu huduma na suluhisho mbalimbali za mawasiliano pamoja na teknolojia za kidijitali, huku wakiwawezesha wananchi kujionea uwezo wa intaneti ya kasi ya juu na huduma zinazolenga matumizi ya nyumbani, taasisi na biashara.

Mbali na elimu hiyo, TTCL imeandaa ofa maalum za Sabasaba zinazowawezesha wateja kupata vifaa vya mawasiliano kwa bei zilizopunguzwa pamoja na huduma mbalimbali za kidijitali zinazorahisisha mawasiliano na shughuli za kila siku.

Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa Banda la TTCL, Bi. Janeth Maeda, alisema ushiriki wa shirika hilo katika Sabasaba 2026 unalenga kuwasogezea wananchi huduma karibu zaidi, kuongeza uelewa kuhusu bidhaa na huduma za TTCL, pamoja na kuimarisha mahusiano na wateja na wadau.

Alisema maonesho hayo pia yanatoa nafasi muhimu kwa TTCL kupokea maoni na mrejesho kutoka kwa wateja ili kuendelea kuboresha huduma zake na kuendana na mahitaji ya soko la mawasiliano linalokua kwa kasi.

Aidha, wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo wanapata fursa ya kutumia huduma ya Public Wi-Fi bila malipo, hatua inayowawezesha kujionea ubora na kasi ya intaneti inayotolewa na TTCL.

TTCL imeendelea kuwahamasisha wananchi kutembelea banda lake katika kipindi chote cha maonesho ili kujionea teknolojia bunifu, kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu huduma za mawasiliano na kunufaika na ofa mbalimbali zilizoandaliwa mahsusi kwa maonesho ya Sabasaba 2026


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...