Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, amesema thamani ya fedha itaendelea kuwa imara kuelekea kipindi cha mavuno ili kuwawezesha wakulima kupata thamani stahiki ya mazao yao kulingana na shughuli za kiuchumi wanazozifanya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) Julai 10, 2026, Tutuba amesema kiwango cha riba ya Benki Kuu cha asilimia 6.25 kinalenga kuhakikisha kunakuwa na utulivu wa bei na mfumuko wa bei unaendelea kubaki kati ya asilimia 3 hadi 5.

Amesema kiwango hicho pia kitawezesha Mabenki kuwa na ukwasi wa kutosha kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa wananchi na wafanyabiashara, hivyo kusaidia shughuli mbalimbali za uzalishaji na biashara nchini.

Tutuba amesema wakulima wanapoanza kuvuna mazao yao, thamani imara ya fedha itasaidia kuhakikisha wanapata malipo yanayolingana na thamani halisi ya mazao yao sokoni.

Ameongeza kuwa wafanyabiashara wanaouza bidhaa nje ya nchi pia watanufaika kwa kupata fedha za kigeni kulingana na thamani ya fedha walizotumia katika uzalishaji, huku tathmini ikionyesha kiwango cha riba cha asilimia 6.25 kinatosha kuendelea kuimarisha shughuli za kiuchumi.

Aidha, amesema BoT hutumia Maonesho ya Sabasaba kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kiwango cha riba ya Benki Kuu katika kudhibiti mfumuko wa bei, kuongeza ukwasi katika mzunguko wa uchumi na kuwezesha upatikanaji wa fedha kwenye mabenki ya biashara.

Tutuba amesema maonesho hayo pia ni fursa kwa Watanzania kujifunza, kupata bidhaa na huduma mbalimbali pamoja na mbinu mpya za kufanya shughuli za kiuchumi zinazochangia ukuaji wa uchumi wa nchi.




Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...