Na Mwandishi Wetu

MECHI kati ya timu ya soka ya Chuo cha Future World na timu ya Chanika Veteran umemalizika kwa sare 1-1 huku ujumbe mkubwa katika mechi hiyo ni kuhamasisha vijana kujiunga na Chuo hicho kupata ujuzi.

Katika mechi hiyo iliyochezwa leo Julai 11,2026 katika uwanja wa VODP uliopo Chanika kata ya zingiziwa wilayani Ilala jijini Dar es Salaam umeshuhudiwa na mamia ya wananchi wa Chanika na viunga vyake.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo Ofisa Masoko kutoka chuo Cha Future World Vocational David Msumba amesema lengo la mechi hiyo ni kukitambulisha chuo kwa wananchi hasa katika kata za Chanika na Zingiziwa

“Tumecheza mechi kati yetu Future World na Chanika Veterani na lengo kuu ni kuhamasisha wananchi kujiunga na chuo chetu ili kupata ujuzi kupitia kozi mbalimbali tunazitoa.”

Ametaja kozi zinazotolewa na chuo hicho ni ufundi wa magari na pikipiki, umeme wa majumbani,ulezi wa watoto wadogo,mafunzo ya urembo na ususi,Hotel Management pamoja na Computer Applications.

“Future World ni chuo chenye uzoefu wa karibu miaka 30 sasa, tangu kilipoanzishwa kwenye utoaji wa Mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali.

“Hivi Karibuni, chuo hiki kimefungua tawi lake jipya eneo la Chanika kwa Ndevu eneo ambalo lina mandhari bora kabisa kwa utoaji wa elimu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa hosteli nzuri za wanafunzi.

“Vijana hasa wahitimu wa kidato cha nne mnakaribishwa chuoni au kuingia kwenye Tovuti ya chuo na kupata fomu ya kujiunga na mafunzo uyapendayo, au kwa mawasiliano 0715 015778 ”amesema Msumba




















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...