WANANCHI wa kijiji cha Ng'ongo kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga wameiomba serikali kuwajengea nyumba watumishi wa Afya na kuongeza wahudumu katika Zahanati ya kijiji hicho huku Zahanati hiyo ikiwa na wahudumu wawili wote wakiwa ni wauguzi hali inayohatarisha Afya za wakazi wa eneo hilo.

Akijibu ombi hilo kwa wananchi Waziri wa katiba na sheria Juma Homera aliwahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa changamoto hiyo itakwenda kutatuliwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na wananchi huku waziri huyo akichangia mifuko 100 ya saruji ili kuanza kwa ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya na kuimarisha huduma za matibabu katika Zahanati hiyo.

Waziri wa katiba na sheria Juma Homera amefungua Zahanati ya kijiji cha Ng'ongo iliyogharim Milioni 120 ikiwa Zahanati hiyo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa milioni 20 huku serikali ikikamilisha ujenzi huo kwa sh. milioni 100.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...