Jane Mwakyoma - Rukwa.

SERIKALI Imewaomba wakulima mkoani Rukwa kuwa na subra ya upandaji wa bei ya mahindi  wakati serikali inapolifanyia kazi suala la bei za mahindi nchini.

Akitoa ufafanuzi huo baada ya mkuu wa wilaya ya Sumbawanga akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Rukwa Nyakia Chirukile baada ya kumuomba Waziri wa katiba na sheria kuhusu serikali kupandisha bei ya mahindi mkoani humo baada ya kukagua ujenzi wa stendi ya mabasi Laela.

Homera amesema serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan inashughulikia changamoto za wananchi katika kuhakikisha wananchi wake wanaondokana na changamoto ya bei ndogo ya mahindi ili kuwainua wakulima kiuchumi.

" Niseme suala la bei ya mazao kila sehemu hii changamoto ipo, ukienda mimi jimbo langu ni Namtumbo, pale wanalima mahindi miongoni mwa mikoa inayolima mahindi ni Ruvuma ,Rukwa, Katavi nadhani na Iringa pia lakini bei ya mahindi huku kwetu imeshuka kwa kiwango kikubwa lakini ndugu zangu niwatoe mashaka hili jambo serikali ya CCM inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan chini ya waziri wa kilimo Daniel Chongoro, inalifahamu kwaiyo tuendelee kuwa na subra kidogo serikali inapolifanyia kazi " amesema Homera.

Pia Homera amesema suala la mbolea serikali ya awamu ya sita inalishughulikia suala hilo na kuwataka wananchi kuendelea kusubili huku serikali ikisisitiza wakulima kuendelea kujiandikisha ili kupata mbolea za ruzuku.

Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria kwa watu wanaotaka kuvuruga amani katika nchi.

Pia amesema wananchi wasikubali kudanganywa kwasababu ya maslahi ya watu wachache na badala yake wahakikishe wanailinda amani ya nchi kwa wivu mkubwa ili kuendelea na shughuli zao za kiuchumi kwa amani na utulivu.

Waziri wa katiba na sheria Juma Homera yupo mkoani Rukwa kwa ziara ya siku nne kwa lengo la kukagua, kutembelea,kuweka mawe ya msingi,kufungua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...