Na Janeth Raphael - MichuziTv
Waandishi wa habari na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wametakiwa kutumia nafasi yao ya kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kufikia lengo la asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2034.
Wito huo umetolewa Julai 16, 2026 mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Habari – MAELEZO, Rodney Mbuya, wakati akifunga warsha ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari na Maafisa Mawasiliano wa Serikali kuhusu uandishi na uhamasishaji wa masuala ya nishati safi ya kupikia.
Mbuya amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeifanya ajenda ya nishati safi ya kupikia kuwa moja ya vipaumbele vya maendeleo kupitia Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa miaka 10 (2024–2034).
Ameeleza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana ambapo matumizi ya nishati safi ya kupikia yamefikia asilimia 28.6 ya kaya nchini, bado kuna haja ya kuongeza juhudi za utoaji wa elimu kwa umma ili kuharakisha mabadiliko ya tabia na kuongeza matumizi ya nishati hiyo salama na rafiki kwa mazingira.
Amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi, kuhamasisha mabadiliko ya mtazamo na kuibua mijadala yenye tija kuhusu faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa afya, mazingira na maendeleo ya kijamii.
Kwa upande mwingine, Bw. Mbuya ameipongeza Wizara ya Nishati, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kupitia Mradi wa CookFund unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya nishati safi ya kupikia kwa kuandaa mafunzo hayo.
Amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo Waandishi wa Habari na Maafisa Mawasiliano wa Serikali kuandaa taarifa zenye ubora na zenye ushawishi, zitakazochochea wananchi wengi zaidi kukumbatia matumizi ya nishati safi ya kupikia na hivyo kuchangia utekelezaji wa ajenda ya Taifa ya nishati safi.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...