Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera, amewataka watumishi wa sekta ya afya nchini kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

Akizungumza Leo Julai 8,2026 wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Afya Kasu kilichopo Kijiji cha Kasu, Kata ya Kandasi, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Dkt. Homera amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuwekeza katika kuboresha huduma za afya kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya kutolea huduma karibu na wananchi.

Amesema ujenzi wa kituo hicho umegharimu takribani shilingi bilioni 1.8, huku Serikali pia ikipanga kujenga barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita moja kuelekea kituoni hapo kwa gharama ya takribani shilingi milioni 500, hatua itakayorahisisha upatikanaji wa huduma za afya.

Wananchi wa eneo hilo wameishukuru Serikali kwa kukamilisha mradi huo, wakieleza kuwa utapunguza umbali waliokuwa wakitembea kufuata huduma za afya na kuboresha huduma za mama na mtoto pamoja na huduma nyingine muhimu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...