Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi inayotekelezwa kupitia mradi wa Uboreshaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP) inazingatia ubora, kasi ya utekelezaji na matumizi sahihi ya fedha za umma.
Prof. Kabudi amesema kuwa fedha zinazotumika katika mradi huo ni mkopo ambao serikali italipa, hivyo ni wajibu wa kila anayehusika na utekelezaji kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa ufanisi na kuleta thamani halisi kwa watanzania.
Pia Prof. Kabudi ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya TARURA wilaya ya Ubungo unaoendelea chini ya mradi huo huku akiwapongeza wakandarasi, washauri elekezi na watendaji wote wanaosimamia utekelezaji wa mradi huo.
Aidha, amewataka washauri elekezi kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ili kuhakikisha kazi zote zinafanyika kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa na thamani ya fedha inaonekana katika kila hatua ya utekelezaji.
Akikagua ujenzi wa barabara ya Kizota- Changanyikeni iliyopo wilayani Kinondoni, Prof. Kabudi amesisitiza umuhimu wa kujenga mifereji ya maji sambamba na barabara, akieleza kuwa kutokuwepo kwa mifereji husababisha maji ya mvua kuharibu barabara mapema na kusababisha hasara kwa serikali.
Sambamba na hilo amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kuepuka kutupa taka hovyo katika mifereji na madaraja.
Amehitimisha kwa kuwapongeza wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Ofisi ya Mkoa, TARURA na wote wanaoshiriki katika utekelezaji wa mradi huo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na weledi ili miradi hiyo ikamilike kwa ubora uliokusudiwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wametoa shukrani zao za dhati kwa serikali kwa ujenzi wa barabara hiyo wakisema imewapandisha hadhi na heshima.



.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...