Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili jijini Paris, Ufaransa leo, Julai 6, 2026, kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yanayofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO.

Mara baada ya kuwasili, Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Thabit Kombo, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Saidi Yakubu na maafisa wengine wa ubalozi.

Katika maadhimisho hayo, Tanzania itaendelea kuonesha nafasi yake ya kipekee katika kukuza, kuhifadhi na kuieneza lugha ya Kiswahili duniani, sambamba na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kupitia lugha hiyo. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...