Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Sheikh Rashid Hamad Othman, Kaka mkubwa wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Othman Masoud Othman, anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam. Akiwa hospitalini hapo Mhe. Rais Dkt. Samia pia alijulishwa kuhusu kuwepo kwa Mchezaji wa Timu ya Yanga Pacome Zouzoua katika chumba jirani, ambapo alipata muda wa kumtembelea na kumpa pole kufuatia majeraha aliyopata katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...