-MACHAFUKO YATAZALISHA WALEMAVU WENGI ZAIDI"
Na Mashaka Mhando, TANGA.
SERIKALI imewatahadharisha Watanzania kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini, ikionya kuwa machafuko na kutovumiliana kisiasa ndio chanzo kikuu cha kuzalisha idadi kubwa ya watu wenye ulemavu.
Tahadhari hiyo nzito imetolewa jana jijini Tanga na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, alipokuwa mgeni rasmi katika hafla kubwa ya ugawaji wa vifaa saidizi vilivyogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 170 kwa watu wenye ulemavu; hafla iliyoandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Mhandisi Mwanaisha Ulenge.
Akizungumza mbele ya mamia ya wakazi wa Jiji la Tanga, Waziri Omar alisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kujenga utamaduni wa kutofautiana kwa mawazo bila kuhitilafiana kimatendo, kwani amani ndio msingi pekee wa maendeleo na ustawi wa jamii.
"Niwaombe tuendelee kudumisha amani yetu. Inapovunjika amani, wanaweza kupatikana walemavu wengi sana katika jamii. Tunaweza kutofautiana kwa mawazo, lakini isiwe sababu ya kuhitilafiana na kuvunja amani yetu," alionya Balozi Omar.
Pamoja na onyo hilo, Waziri Omar alitumia wasaa huo kumwagia sifa Mhandisi Ulenge kwa hatua yake ya kiungwana ya kuifikiria na kuigusa jamii ya watu wenye ulemavu, akieleza kuwa msaada huo unaimarisha utu wao na kuwapa fursa ya kuishi kwa kujitegemea na kuondokana na hofu ya kimaisha.
Mamilioni ya Vifaa Saidizi na Mafunzo ya PPRA
Awali, akisoma risala yake kwa mgeni rasmi, Mhandisi Mwanaisha Ulenge alibainisha kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya mamilioni ya fedha vimetolewa kupitia ufadhili wa Taasisi ya Kamal Foundation.
Alivitaja vifaa vilivyogawiwa kuwa ni pamoja na:
* Viti mwendo (Wheelchairs): 31
* Miguu bandia: 100
* Fimbo za wasioona: 25
Mhandisi Ulenge alifafanua kuwa, ili kuhakikisha walemavu hao hawabaki nyuma kiuchumi, walipatiwa pia elimu maalum ya manunuzi ya umma kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Hatua hiyo inalenga kuwawezesha makundi hayo maalum kushiriki kikamilifu katika fursa za kiuchumi na kupata tenda za Serikali ili kuongeza tija kwenye kazi zao.
Aidha, Mbunge huyo alitumia jukwaa hilo kuiomba Serikali kupitia Waziri wa Fedha kuharakisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi ya kimkakati mkoani humo, akiangazia zaidi umuhimu wa barabara ya Tanga–Pangani.
Vigogo wa CCM Watoa Neno
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga, Meja (Mst) Hamisi Mkoba, alieleza kuwa msaada huo mkubwa uliotolewa na Mbunge huyo ni sadaka yenye thamani kubwa isiyopimika.
"Haya yote tunayoyafanya leo ni kwa sababu nchi ina amani. Tuendelee kudumisha amani yetu. Hii ndiyo sadaka bora duniani," alisisitiza Meja Mstaafu Mkoba.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tanga, Hajat Sheymar Kweigir, alihitimisha kwa kueleza kuwa hatua iliyochukuliwa na Mhandisi Ulenge inaakisi kwa vitendo maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha makundi yenye mahitaji maalum nchini yanapata huduma bora na fursa stahiki.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...