Na Mashaka Mhando, Tanga
Hatimaye, Mzee Mohamed Rashid Mkwaje, ambaye aliondoka nyumbani kwao tangu mwaka 1974 kwenda kufanya kazi ya kukata mkonge wilayani Muheza, amefanikiwa kurejea na kuungana tena na familia yake katika Kijiji cha Ligunga, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, baada ya kupita miaka 52.
Mzee huyo amepokelewa kwa hisia kali na vilio vya furaha, hasa kutoka kwa mama yake mzazi, Asmin Kandulu ambaye alikuwa amekata tamaa na kutokuwa na uhakika kama mwanaye alikuwa bado hai baada ya ukimya wa zaidi ya nusu karne.
Kufuatia mapokezi hayo, wajukuu na ndugu wengine wa familia walimfanyia matambiko maalum ya kimila yaliyoambatana na nyimbo za asili za kabila la Kihiyao, ikiwa ni ishara ya kumpokea na kusherehekea kurejea kwa mtoto wao aliyekuwa amepotea.
Safari ya kurejea kwa Mzee Mkwaje ilianza Alhamisi Augosti 20 akitokea Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, ambapo alisindikizwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wa wilaya hiyo, Silvanus Misigaro.
Akizungumza baada ya kufanikisha safari hiyo, Misigaro alisema walimkabidhi mzee huyo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Alfred Rwechungura pamoja na Ofisa Ustawi wa eneo hilo, ambao walishirikiana kumfikisha hadi kijijini kwao Ligunga.
"Alipokelewa na mama yake mzazi Asmina, kiukweli mama yake alilia sana kwa kumkosa mtoto wake kwa miaka mingi. Alikuwa na hisia sana na hakuwa na uhakika kama mwanaye huyu bado alikuwa hai," alisema Misigaro akisimulia tukio hilo la kusisimua.
Awali, Mzee huyo ambaye alikuwa akiishi Kijiji cha Ngomeni wilayani Muheza bila familia yoyote, alifika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza kuomba msaada wa nauli ya kumrudisha kwao. Kufuatia maombi hayo, ofisi hiyo ilimpatia kibali maalum cha kuchangisha fedha za hiari (Kumb. Na. DC/MUH/S.20/VOL. VIII/232) kilichoanza kutumika Agosti 10 mwaka huu.
Hata hivyo, wakati Mzee Mkwaje akiwa amefanikiwa kuchangisha kiasi cha Shilingi 30,000 pekee kupitia kibali hicho, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, aliguswa na mkasa huo na kutoa msaada wa Shilingi 200,000 kwa ajili ya nauli, fedha zilizokabidhiwa kupitia kwa Mwandishi wa Habari, Mashaka Mhando, ambaye naye alimkabidhi Ofisa Ustawi, Misigaro.
Akizungumza kwa furaha baada ya kufika nyumbani na kuonana na wapendwa wake, Mzee Mkwaje alitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Wilaya ya Muheza na Tunduru, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, na watu wote waliojitolea kwa namna moja au nyingine kuhakikisha anatimiza ndoto ya kuonana tena na mama yake tangu alipoondoka kwenda kwenye mashamba ya mkonge miongo mitano iliyopita.
"Naishukuru serikali kusema kweli, wameniheshimisha, sikuwa nina uhakika kama kweli nitarudi nyumbani, niliona kama jambo ambalo haiwezekani kutokana na kwamba nilikuwa naona sieleweki ombi nililokuwa nataka kurudi nyumbani, nawashukuru wote waliohusika na hili," alisema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...