Na Paul Kayanda, Kahama
DIWANI wa Kata ya Majengo, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Zacharia Shida Soko, ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kuboresha sekta ya elimu katika kata hiyo baada ya kukabidhi mashine ya photocopy yenye thamani ya shilingi milioni 3.5 pamoja na karatasi (LIMU) kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa mitihani katika Shule ya Msingi Anderson Msumba.
Mbali na mashine hiyo, Diwani Soko ametoa kiasi cha shilingi 600,000 kwa ajili ya kuwalipa walimu watatu wanaojitolea kufundisha katika shule hiyo, hatua inayolenga kuongeza nguvu kazi ya walimu na kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira bora.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Soko amesema dhamira yake ni kuhakikisha Kata ya Majengo inafanya vizuri katika Manispaa ya Kahama, hususan katika sekta ya elimu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya jamii.
“Kazi ni kuhakikisha Majengo inafanya vizuri katika Manispaa ya Kahama,” amesema Diwani Soko, huku akisisitiza kuwa atandelea kushirikiana na wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha changamoto za elimu zinatatuliwa.
Amewataka wanafunzi kujifunza kwa bidii na kuzingatia nidhamu shuleni na nyumbani, akisema wazazi wao wanahangaika na kujitoa kwa ajili ya kuhakikisha watoto wanapata elimu na baadaye kutimiza ndoto zao.
Soko amesema mafanikio katika jambo lolote, iwe katika elimu au biashara, yanahitaji nidhamu, hivyo amewataka wanafunzi kuifanya nidhamu kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Katika kuhamasisha nidhamu na maadili, Diwani Soko ametangaza kuwa wanafunzi kumi watakaofanya vizuri katika suala la nidhamu shuleni watapatiwa zawadi, akisema hatua hiyo inalenga kuendeleza utamaduni wa nidhamu na maadili mema shuleni na nyumbani.
Hata hivyo Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Sokola, Henry Mika Mayunga, amemshukuru Diwani Soko kwa hatua hiyo, akisema amekuwa msaada mkubwa kwa watoto katika shule za Kata ya Majengo, ikiwemo Anderson Msumba, Majengo na Mama Samia Sekondari.
Mayunga amesema Diwani huyo amekuwa akichangia pia upatikanaji wa chakula katika shule za kata yake, huku akieleza kuwa makabidhiano ya mashine hiyo yameondoa usumbufu uliokuwa ukiwakabili wazazi wa kuchangishwa fedha na watoto kwa ajili ya kutengeneza nakala za mitihani.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokola, Patrobas Privatus, amesema Diwani Soko amekuwa akihakikisha kiwango cha elimu kinaongezeka katika shule za kata hiyo, akiamini kuwa mashine hiyo itasaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Privatus amemuomba Diwani huyo pia kushirikiana na viongozi wa dini kuwaleta walimu wa dini mbalimbali shuleni ili wanafunzi wapate malezi ya kiroho na maadili, akisisitiza kuwa suala la maadili linapaswa kupewa uzito katika malezi ya watoto.
Aidha, ameomba serikali inapotenga na kujenga shule mpya izingatie pia uwepo wa vyumba maalumu kwa ajili ya mafundisho ya dini, akisema hatua hiyo inaweza kusaidia katika kujenga kizazi chenye maadili mema.
Katibu wa CCM Kata ya Majengo, Sebabistian Masonga, amemtaka Diwani Soko kutokata tamaa katika juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo, akiahidi kuwa chama kitaendelea kumuunga mkono kutokana na uchapakazi wake. Amesema vifaa na fedha alizokabidhi shuleni vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne.
Masonga amesema Kata ya Majengo imewahi kuongozwa na madiwani mbalimbali, lakini haijawahi kuona kasi ya maendeleo kama ilivyo sasa.
Ameongeza kuwa ombi la mashine hiyo liliwasilishwa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kahama, Benjamin Ngayiwa, lakini Diwani Soko ameonyesha uwezo wa kulitatua kwa kulifanyia kazi moja kwa moja.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Anderson Msumba, Scholastica Leonard, amesema msaada huo utawafanya wanafunzi kufanya mitihani bila kuchangishwa fedha na wazazi.
Amesema awali wazazi walikuwa wakichangia fedha za mitihani na karatasi, hali iliyosababisha baadhi ya wanafunzi kurudishwa nyumbani kutafuta fedha na hatimaye kuchangia utoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Saidi Kishimba John, amesema “kilio” chao kimepata suluhu na sasa wanailenga Anderson Msumba kupata matokeo ya daraja A, huku akisisitiza umuhimu wa nidhamu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...