Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndugu Wazo Michael Mwang’onda, leo tarehe 28 Agosti 2026 amezindua rasmi kituo kipya cha Polisi cha Musasa kilichopo Kata ya Runzewe Magharibi, Wilaya ya Bukombe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mwang’onda amewapongeza uongozi wa Musasa Gold Mine kwa kugharamia ujenzi wa kituo hicho na kuiomba jamii kuendelea kushirikiana na wawekezaji katika kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi wa Polisi Safia Jongo, amesema kituo hiki ndicho kitakuwa kikuu kwa Kata yote ya Runzewe. Amesema wananchi wa Musasa na Runzewe kwa ujumla watahudumiwa huduma zote za kipolisi kupitia kituo hicho.

Ujenzi wa kituo hiki ulianza tarehe 16 Machi 2026 na umegharimu *shilingi 150,000,000. Kati ya hizo shilingi 145,000,000 zimetolewa na Musasa Gold Mine huku wananchi wakichangia shilingi 5,000,000 kupitia nguvu zao. Mgodi pia umenunua samani zote za ofisi.

Uanzishwaji wa kituo hiki umetokana na ongezeko la watu katika eneo hilo kutokana na shughuli za uchimbaji madini. Viongozi wamesema uwepo wake utasaidia kuimarisha ulinzi, kupunguza uhalifu, kutoa mwitikio wa haraka na kukuza mazingira salama kwa uwekezaji.

Wananchi wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita na wawekezaji kwa hatua hiyo na wameahidi kulinda miundombinu hiyo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...