Na Belinda Joseph-Dodoma.
Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Mbinga (MBIFACU) mkoani Ruvuma kinatarajia kukusanya tani 27,000 za kahawa katika msimu wa mwaka 2026/2027, ikiwa ni ongezeko kutoka tani 24,000 zilizokusanywa msimu wa 2025/2026, kufuatia kuongezeka kwa mashamba yaliyopandwa miaka miwili iliyopita pamoja na wakulima wengi kuhamasika kuboresha mashamba yao kutokana na matarajio ya kuendelea kuwepo kwa bei nzuri ya kahawa sokoni.
Akizungumza katika Maonesho ya Kilimo Nanenane Kitaifa yanayoendelea jijini Dodoma, Agosti 3, 2026, Meneja Mkuu wa MBIFACU, Faraja Komba, amesema katika msimu wa 2025/2026 chama hicho kilisimamia uzalishaji wa tani 24,000 za kahawa kupitia vyama vya ushirika vinavyounda MBIFACU na kahawa hiyo iliuzwa kwa wastani wa shilingi 12,000 kwa kilo na kuwaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 282 zilizolipwa moja kwa moja, jambo lililowawezesha kupata faida kubwa kutokana na bei nzuri ya kahawa.
Amesema matarajio ya kukusanya tani 27,000 msimu huu yanatokana na mashamba yaliyopandwa miaka miwili iliyopita kuanza kuvunwa pamoja na wakulima wengi kuhamasika kuboresha mashamba yao, ameongeza kuwa matarajio ya bei ya kahawa yanaendelea kuwa mazuri kutokana na ubora wa kahawa inayozalishwa na wakulima wa MBIFACU.
Akizungumzia kaulimbiu ya Nanenane 2026 isemayo "Tambua Soko, Zalisha kwa Tija na Tekeleza Dira ya Taifa ya 2050," amesema MBIFACU imeamua kushiriki maonesho hayo ili kutangaza bidhaa zake, kutafuta masoko mapya na kuwafikia wadau mbalimbali wa sekta ya kahawa, amesema chama hicho huzalisha kahawa aina ya Arabica katika Wilaya ya Mbinga kwa wastani wa tani kati ya 25,000 na 30,000 kila mwaka.
Aidha, ameeleza kuwa MBIFACU inaendelea kuwahamasisha wakulima kuzalisha kwa tija kwa kuzingatia ubora wa mazao kuanzia shambani, kuongeza uzalishaji kulingana na ukubwa wa mashamba na kupunguza gharama za uzalishaji ili kuongeza kipato cha mkulima.
Pia amesema kupitia banda la MBIFACU katika maonesho hayo, wakulima na wananchi wanapata elimu kuhusu uzalishaji bora wa kahawa na mbinu za kuongeza thamani ya zao hilo, huku chama hicho kikijipanga kuwashirikisha zaidi wanawake na vijana katika uzalishaji wa kahawa ili kutekeleza Dira ya Taifa ya 2050.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa MBIFACU, Osmund Mbunda, amesema chama hicho kimefanikiwa kuongeza thamani ya kahawa kwa kusindika na kuuza kahawa iliyotayari kwa matumizi badala ya kuuza kahawa ghafi pekee, amesema MBIFACU huuza kahawa kavu, kahawa safi na kahawa iliyoongezwa thamani kwa kusindikwa, huku ikiendelea kuwahamasisha wakulima kutumia kahawa zaidi badala ya chai.
Mbunda amebainisha kuwa, ubora wa kahawa unaanzia shambani na siyo sokoni, hivyo wakulima wanapaswa kuzingatia kanuni bora za uzalishaji tangu hatua za awali.
Ameongeza kuwa lengo la MBIFACU ni kuhakikisha Wilaya ya Mbinga na Mkoa wa Ruvuma vinaendelea kuongoza uzalishaji wa kahawa aina ya Arabica nchini ifikapo mwaka 2050, akibainisha kuwa kwa sasa Ruvuma ndiyo mkoa unaoongoza kwa uzalishaji wa Arabica nchini na unashika nafasi ya pili kitaifa kwa uzalishaji wa kahawa baada ya Mkoa wa Kagera unaozalisha kahawa aina ya Robusta.
Kwa upande wake, Mrajis wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Ruvuma, Venance Msafiri, amesema wakulima wa kahawa mkoani Ruvuma wameendelea kunufaika na mauzo ya kahawa kupitia vyama vya ushirika, hali iliyochangia kuongeza kipato cha wakulima mmoja mmoja na kuboresha uchumi wa mkoa kwa ujumla.
Amesema mfumo wa ushirika umeendelea kuwawezesha wakulima kupata soko la uhakika, malipo kwa wakati na bei nzuri ya kahawa, jambo lililoongeza ari ya wakulima kuendelea kuwekeza katika uzalishaji wa zao hilo, aidha amewahimiza wakulima kuendelea kutumia vyama vya ushirika kama chombo cha kuimarisha masoko ya mazao yao na kuongeza tija katika uzalishaji wa kahawa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...