NA DENIS MLOWE IRINGA
MEYA wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada, amefuta taarifa iliyokuwa imeeleza kuwa Halmashauri imekubaliana kuongeza ada katika shule za mchepuo wa Kiingereza, ikiwemo Shule ya Msingi Mapinduzi, kutoka Shilingi 300,000 hadi Shilingi 500,000 kwa mwaka.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Meya Ngwada alisema suala la kuongeza ada halijapitishwa na kwamba kumbukumbu zilizowasilishwa zilikuwa na taarifa isiyoendana na uamuzi wa kikao.
Alisema awali wataalamu walipewa jukumu la kufanya upembuzi na kuwasilisha mapendekezo kuhusu uwezekano wa kubadili ada, na kwamba suala hilo linapaswa kurejea katika vikao halali vya kisheria kabla ya uamuzi wowote kufanyika.
“Hatujapandisha ada kwenye shule zetu za Mapinduzi, Gangilonga na Chifu Mkwawa. zitabaki kuwa zile zile hatujabadilisha ada,” alisema Meya Ngwada.
Meya Ngwada aliwataka wazazi na wananchi kutokuwa na hofu, akisisitiza kuwa kwa sasa hakuna ongezeko la ada lililoidhinishwa katika shule hizo na endapo kutakuwa na umuhimu wa kufanya mabadiliko, suala hilo litajadiliwa na kuamuliwa kupitia taratibu za kisheria.
Baraza hilo pia lilijadili hoja kuhusu uamuzi wa kuhamisha Shule ya Msingi Ilala kuwa chini ya Chuo Kikuu cha Mkwawa ambapo Meya Ngwada alisema uamuzi huo umempa maswali, hasa baada ya kupata maelezo kuwa pamoja na shule hiyo, ardhi ilipojengwa pia itahamishwa.
Alisema Chuo Kikuu cha Mkwawa kina eneo kubwa linalozidi ekari 600, hivyo kwa mtazamo wake kungekuwa na uwezekano wa kutenga eneo ndani ya chuo hicho na kujenga shule mpya badala ya kuhamisha ardhi ya shule hiyo kutoka katika umiliki wa Halmashauri.
Meya Ngwada alisisitiza kuwa hoja yake haikuwa ya kupinga uamuzi ambao tayari umepitishwa na vikao vya Halmashauri, bali alikuwa akiweka wazi wasiwasi wake kuhusu umiliki wa ardhi na namna rasilimali hiyo inavyoweza kutumika kwa manufaa ya wananchi
Kwa upande mwingine, Diwani Likotiko Kenyatta alihoji utekelezaji wa mpango wa Halmashauri wa kufanya mazungumzo na Chama Cha Mapinduzi kuhusu eneo la Sabasaba.
Akijibu hoja hiyo, Ngwada alileza kuwa eneo hilo linamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi na lina hati ya umiliki halmashauri imependekeza kufanyika kwa mabadilishano ya maeneo ili eneo hilo liweze kubaki chini ya matumizi ya wananchi.
Eneo la Sabasaba lina Shule ya Msingi, shule ya mahitaji maalum pamoja na kituo cha afya, hivyo Halmashauri imesema inaona umuhimu wa kupata umiliki wa eneo hilo ili iweze kuendelea kufanya uwekezaji katika huduma hizo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...