Na Belinda Joseph-Tanga
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inatekeleza Mradi wa Elimu na Stadi kwa Ajira zenye Tija Awamu ya Pili (ESPJ II), unaolenga kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi nchini kupitia uanzishaji wa vituo 15 vya umahiri katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza katika Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Meneja Uhusiano na Masoko kutoka VETA Sitta Peter, amesema mradi huo ni sehemu ya hatua za Mamlaka hiyo kupanua mafunzo ya ufundi stadi na kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.
Amesema vituo hivyo vitajikita katika maeneo maalumu ya mafunzo na umahiri, hatua inayolenga kuongeza ubora wa mafunzo na kuwaandaa wahitimu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa viwango vinavyohitajika katika sekta mbalimbali kwenye soko la ajira kimataifa.
Amewahimiza wananchi kutumia fursa ya maonesho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kutembelea banda la VETA na kupata taarifa kuhusu kozi zinazotolewa, hasa kwa kuwa maombi ya mafunzo ya muda mrefu yanaendelea kupokelewa.
Amesema VETA ni kwa ajili ya Watanzania wote yaani wenye viwango tofauti vya elimu, kuanzia waliomaliza elimu ya msingi hadi wenye shahada na shahada za uzamili, hivyo wananchi wanapaswa kuchagua stadi wanayoona inaweza kuwasaidia katika ajira au kujiajiri.
Ameeleza kuwa gharama za mafunzo ni nafuu, ambapo mwanafunzi wa kutwa hulipa shilingi 60,000 kwa mwaka, huku anayekaa bweni akilipa shilingi 120,000 kwa mwaka, bila kujumuisha baadhi ya mahitaji binafsi na vifaa vya usalama vinavyohitajika katika mafunzo ya vitendo.
Aidha, Sitta amewahimiza watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa hiyo, kwa kuwa wanafunzi wenye ulemavu wanaodahiliwa kujiunga na VETA wanalipiwa malipo ya ada na Mamlaka hiyo, hivyo wao wanatakiwa kugharamia mahitaji yao binafsi na sio ada.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...